\v 22 Kwa hiyo watu wakasafiri kutoka Kadeshi. Wana wa Israeli, watu wote, wakafika Mlima Hori. \v 23 BWANA akanena na Musa na Haruni hapo kwenye Mlima Hori, kwenye mpaka wa Edomu. Akasema, \v 24 "Sasa ni wakati wa Haruni kukusanyika na watu wake, hataingia katika nchi ile niliyowaahidi wana wa Israeli. Hii ni kwa sababu ninyi wawili hamkuitii sauti yangu pale kwenye maji ya Meriba.