sw_neh_text_reg/09/32.txt

1 line
554 B
Plaintext

\v 32 Basi, Mungu wetu, Mungu wetu mkuu, mwenye nguvu na mwenye kutisha, unayeweka agano lako na upendo wako, shida zote zilizotupata sisi, wafalme wetu, wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na baba zetu, na watu wako wote tangu siku za wafalme wa Ashuru mpaka leo usizihesabu kuwa ni kidogo. \v 33 Wewe ni mwenye haki katika yote yaliyotupata, kwa kuwa umetenda kwa uaminifu, na tumefanya uovu. \v 34 Wafalme wetu, wakuu wetu, makuhani wetu, na baba zetu hawakuishika sheria yako, wala hawakuzingatia amri zako au shuhuda zako ulizowashuhudia.