sw_neh_text_reg/09/28.txt

1 line
493 B
Plaintext

\v 28 Lakini baada ya kupumzika, wakafanya mabaya tena mbele yako, nawe ukawaacha mikononi mwa adui zao, kwa hiyo adui zao wakatawala juu yao. Hata walipokurudia na kukulilia, ukasikia kutoka mbinguni, mara nyingi ukawaokoa kwa sababu ya huruma yako. \v 29 Uliwaonya ili wapate kurudi kwenye sheria yako. Hata hivyo walifanya kiburi na hawakusikiliza amri zako. Walifanya dhambi dhidi ya amri zako ambazo humpa uzima mtu yeyote anayezitii. Hawakuzitii, hawakuzitenda na walikataa kuzisikiliza.