sw_neh_text_reg/09/03.txt

1 line
317 B
Plaintext

\v 3 Walisimama mahali pao, na robo ya siku walisoma kutoka Kitabu cha Sheria ya Bwana Mungu wao. Na robo nyingine ya siku walikiri na kuinama mbele ya Bwana Mungu wao. \v 4 Walawi, Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebaniya, Buni, Sherebia, Bani na Kenani, walisimama juu ya ngazi, wakamwita Bwana, Mungu wao kwa sauti kubwa.