sw_neh_text_reg/10/28.txt

1 line
511 B
Plaintext

\v 28 Na watu wengine waliokuwa makuhani, na Walawi, na walinzi wa malango, na waimbaji, na watumishi wa hekalu, na wote waliokuwa wamejitenga wenyewe na watu wa nchi za jirani, kwa sheria ya Mungu, na wanawake zao, na wana wao, na Binti zao, wote walio na ujuzi na ufahamu, \v 29 walijiunga na ndugu zao, wakuu wao, na kujifunga katika laana na kiapo cha kutembea katika sheria ya Mungu, iliyotolewa na Musa mtumishi wa Mungu, na kuzingatia na kutii amri zote za Bwana Mungu wetu na hukumu zake na sheria zake.