sw_neh_text_reg/12/24.txt

1 line
526 B
Plaintext

\v 24 Wakuu wa Walawi walikuwa Hashabia, Sherebia, na Yeshua mwana wa Kadmieli, pamoja na washirika wao, waliokuwa wamesimama mbele yao kumtukuza na kumshukuru, akijibu sehemu kwa sehemu, kwa kutii amri ya Daudi, mtu wa Mungu. \v 25 Matania, Bakbukia, Obadiya, Meshulamu, Talmoni na Akubu walikuwa walinzi wa malango waliokuwa wakiwa wamesimama katika vyumba vya hazina penye malango. \v 26 Walitumika katika siku za Yoyakimu, mwana wa Yoshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za Nehemiya, gavana na Ezra kuhani na mwandishi.