sw_neh_text_reg/09/05.txt

1 line
491 B
Plaintext

\v 5 Ndipo Walawi, na Yeshua, na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethalia, wakasema, "Simameni, mkamsifu Bwana, Mungu wenu, milele na milele." "Libarikiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote. \v 6 Wewe ni Bwana. Wewe peke yako. Wewe umefanya mbinguni, mbingu za juu, na malaika wote wa vita vita, na dunia na kila kitu kilicho juu yake, na bahari na vyote vilivyomo. Unawapa wote uzima, na majeshi ya malaika wanakusujudia.