sw_neh_text_reg/03/01.txt

1 line
284 B
Plaintext

\v 1 Kisha Eliashibu, kuhani mkuu, akasimama pamoja na ndugu zake makuhani, wakajenga lango la kondoo. Walitakasa na kuweka milango yake. Waliweka wakfu hadi mnara wa Hamea na hadi mnara wa Hananeli. \v 2 Baada yao watu wa Yeriko walijenga, na baada yao Zakuri mwana wa Imri alijenga.