sw_mrk_text_ulb/14/66.txt

1 line
423 B
Plaintext

\v 66 Na Petro alipokuwa bado yuko chini uani, mtumishi mmoja wa wasichana wa kuhani mkuu alikuja kwake. \v 67 Alimwona Petro alipokuwa amesimama akiota moto, na alimtazama kwa kumkaribia. Kisha alisema, "Nawe pia ulikuwa na Mnazareti, Yesu". \v 68 Lakini alikataa, akisema, "Sijui wala sielewi kuhusu kile unachosema!" Kisha alitoka akaenda nje uani. (Zingatia; Mstari huu, "Na jogoo akawika" haumo kwenye nakala za kale).