sw_mrk_text_ulb/14/40.txt

1 line
324 B
Plaintext

\v 40 Alikuja tena akawakuta wamelala, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito na hawakujua nini cha kumwambia. \v 41 Alikuja mara ya tatu na kuwaambia, "Bado mmelala na kupumzika? Yatosha! Saa imefika. Tazama! Mwana wa Adamu atasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi. \v 42 Amkeni, twendeni. Tazama, yule anayenisaliti yuko karibu."