sw_mrk_text_ulb/14/22.txt

1 line
404 B
Plaintext

\v 22 Na walipokuwa wakila, Yesu alichukua mkate, akaubariki, na kuumega. Aliwapa akisema, "Chukueni. Huu ni mwili wangu." \v 23 Alichukua kikombe, akashukuru, na akawapatia, na wote wakakinywea. \v 24 Aliwaambia, "Hii ni damu yangu ya agano, damu imwagikayo kwa ajili ya wengi. \v 25 Kweli nawaambia, sitakunywa tena katika zao hili la mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika ufalme wa Mungu."