sw_mrk_text_ulb/14/03.txt

1 line
458 B
Plaintext

\v 3 Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akielekea mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa na chupa ya marashi ya nardo safi yenye gharama kubwa sana, aliivunja chupa na kuimimina juu ya kichwa chake. \v 4 Lakini kulikuwa na baadhi yao waliokasirika. Waliambiana wao kwa wao wakisema, "Ni nini sababu ya upotevu huu? \v 5 Manukato haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na wakapewa maskini." Nao walimkemea.