sw_mrk_text_ulb/13/24.txt

1 line
400 B
Plaintext

\v 24 Lakini baada ya mateso ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, \v 25 nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu zilizoko mbinguni zitatikisika. \v 26 Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu kubwa na utukufu. \v 27 Ndipo atatuma malaika zake na atawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande kuu nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.