1 line
461 B
Plaintext
1 line
461 B
Plaintext
\v 1 Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mifano. Akasema, "Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la kusindika mvinyo. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali. \v 2 Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu. \v 3 Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote. |