sw_mrk_text_ulb/10/46.txt

1 line
378 B
Plaintext

\v 46 Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara. \v 47 Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianza kupiga kelele na kusema, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!" \v 48 Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"