sw_mrk_text_ulb/10/17.txt

1 line
365 B
Plaintext

\v 17 Na alipoanza safari yake mtu mmoja alimkimbilia na akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niweze kurithi uzima ya milele?" \v 18 Na Yesu akasema, "Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema, isipokuwa Mungu peke yake. \v 19 Unazijua amri: 'Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, mheshimu baba na mama yako'."