sw_mrk_text_ulb/08/11.txt

1 line
364 B
Plaintext

\v 11 Kisha Mafarisayo walitoka nje na kuanza kubishana naye. Walitaka awape ishara kutoka mbinguni, kwa kumjaribu. \v 12 Akatafakari kwa kina moyoni mwake akasema, "Kwa nini kizazi hiki kinatafuta ishara? Nawaambia ninyi kweli, hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki." \v 13 Kisha akawaacha, akaingia ndani ya mashua tena, akaondoka kuelekea upande mwingine.