sw_mrk_text_ulb/08/01.txt

1 line
444 B
Plaintext

\v 1 Katika siku hizo, kulikuwa tena na umati mkubwa, na hawakuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, \v 2 "Ninauhurumia umati huu, wameendelea kuwa nami kwa siku tatu na hawana chakula. \v 3 Nikiwatawanya warudi majumbani kwao bila kula wanaweza wakazimia njiani kwa njaa. Na baadhi yao wametoka mbali sana." \v 4 Wanafunzi wake wakamjibu, "Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwashibisha watu hawa katika eneo hili lililoachwa?"