\v 10 Na akawaambia, "Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka. \v 11 Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao."