1 line
409 B
Plaintext
1 line
409 B
Plaintext
\v 15 Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Mlawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata. \v 16 Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, "Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?" |