sw_mrk_text_ulb/08/01.txt

1 line
489 B
Plaintext

\c 8 \v 1 Katika siku hizo, kulikuwa tena na umati mkubwa, na hawakuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake na akawaambia, \v 2 "Nina huruma kwa umati huu, kwa sababu wameendelea kuwa nami tayari kwa siku tatu na hawana chakula. \v 3 Nikiwaacha warudi majumbani mwao bila kula wanaweza wakazimia njiani kwa njaa. Na baadhi yao wametoka mbali sana." \v 4 Wanafunzi wake wakamjibu, "Tutaweza kupata wapi mikate ya kutosha katika sehemu kama hii isiyo na watu ili kuwashibisha watu hawa?"