sw_mrk_text_ulb/11/01.txt

1 line
438 B
Plaintext

\c 11 \v 1 Sasa walipokuwa wakifika Yerusalemu, walikuwa karibu na Bethfage na Bethania, kwenye Mlima wa Mizeituni, Yesu akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake \v 2 na akawaambia, "Nendeni katika kijiji kinyume na sisi. Mara mtakapoingia humo, mtamkuta mwanapunda ambaye hajapandwa. Mfungueni na mmlete kwangu. \v 3 Na kama yeyote akiwaambia, 'Kwa nini mnafanya hivi'?, mnapaswa kusema, 'Bwana anamhitaji na mara atamrudisha hapa'."