sw_mrk_text_ulb/05/25.txt

1 line
438 B
Plaintext

\v 25 Wakiwa njiani wakienda kwa Yeiro. Kulikuwa na mwanamke ambaye damu yake ilikuwa inamtoka kwa miaka kumi na miwili. \v 26 Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho. Hata hivyo hakupata msaada kwa chochote, lakini siku baada ya siku hali yake ilizidi kuwa mbaya. \v 27 Alisikia habari za Yesu. Hivyo alikuja nyuma ya Yesu wakati alipokuwa akitembea ndani ya umati, naye aliligusa vazi lake.