sw_mrk_text_ulb/05/21.txt

1 line
502 B
Plaintext

\v 21 Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine, ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika kumzunguka, alipokuwa kando ya bahari. \v 22 Na mmoja wa kiongozi wa sinagogi, aliyeitwa Yairo, alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake. \v 23 Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, " Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili aweze kupata afya na kuishi." \v 24 Hivyo alikwenda pamoja naye, na umati wa wanafunzi ulimfuata nao walimzonga karibu wakimzunguka.