\v 9 Pilato akawajibu na kusema, "Mnataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?" \v 10 Kwa kuwa alijua ni kwa sababu ya wivu wakuu wa makuhani walimkamata Yesu na kumleta kwake. \v 11 Lakini wakuu wa makuhani walichochea umati kupiga kelele kwa sauti kwamba afunguliwe Baraba badala yake.