\v 18 Na alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, mtu aliyekuwa akipagawa na mapepo aliomba kwamba aende pamoja naye. \v 19 Lakini hakumruhusu, lakini alimwambia, "Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako, na uwaambie alichokufanyia Bwana, na huruma aliyokupa." \v 20 Hivyo alienda na alianza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake maeneo yote ya Dekapoli, na kila mmoja alistaajabu.