sw_mic_text_reg/07/01.txt

1 line
415 B
Plaintext

\v 1 Ole wangu! Kwangu mimi ni kama msimu wa mavuno ulipokwisha, na pia makombo ya mavuno ya zabibu kwenye shamba la mizabibu: Hakuna tena kishamba cha matunda kinachoonekana, hakuna matini ya malimbuka ambayo ninayoyatamani. \v 2 Watu waaminifu wamepotelea kutoka kwenye nchi, hakuna mtu mwadilifu katika wanadamu wote. Wote hudanganya katika kusubiri kumwaga damu; kila mtu humuwinda ndugu yake mwenyewe kwa wavu.