sw_mic_text_reg/03/09.txt

1 line
439 B
Plaintext

\v 9 Sasa sikieni hii, ninyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, na watawala wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao mnaochukia haki, na kupotosha kila haki. \v 10 Mnaijenga Sayuni kwa damu na Yerusalemu kwa uovu. \v 11 Viongozi wenu huhukumu kwa rushwa, makuhani wenu hufundisha kwa hijara, na manabii wenu hufanya utabiri kwa ajili ya pesa. Hata hivyo bado mtamtegemea Yahwe na kusema, "Je hayupo Yahwe pamoja nasi? Hakuna uovu utakaokuja juu yetu."