sw_lev_text_reg/19/05.txt

1 line
466 B
Plaintext

\v 5 Unapotoa dhabihu za sadaka ya ushirika kwa Yahweh, utatoa ili kupata kibali. \v 6 Ni sharti iliwe siku hiyo hiyo uliyoitoa, au siku inayofuata. \v 7 Kama kinabaki kitu cho chote hata siku ya tatu ni lazima kiteketezwe kwa moto. Kama kitaliwa katika siku ya tatu kitakuwa najisi. Hakitakubalika, \v 8 lakini kila akilaye ni lazima atachukua hatia yake kwa sababu amekivunjia heshima kilicho kitakatifu kwa Yahweh. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.