sw_lev_text_reg/23/17.txt

1 line
554 B
Plaintext

\v 17 Mtaleta kutoka nyumbani mwenu mikate miwili iliyotengenezwa kutokana na mbili za kumi za efa. Ni lazima ifanywe kwa unga laini na uliochanganywa na hamira; zitakuwa matoleo ya kutikiswa ya malimbuko ya kwanza kwa Yahweh. \v 18 Mtaileta hiyo mikate pamoja na wana—kondoo saba wa mwaka mmoja na wasiokuwa na dosari, fahali mmoja mchanga na dume wa kondoo wawili. Watakuwa matoleo ya kuteketezwa kwa moto kwa Yahweh, pamoja na matoleo yao ya nafaka na matoleo ya kinywaji, matoleo yaliyofanywa kwa moto na kutoa harufu nzuri ya kupendeza kwa Yahweh.