sw_lev_text_reg/21/22.txt

1 line
400 B
Plaintext

\v 22 Anaweza kula chakula cha Mungu wake, ama iwe baadhi ya vile vilivyo vitakatifu sana au vile vitakatifu. \v 23 Hata hivyo, hataingia ndani ya pazia wala kuisogelea madhabahu, kwa sababu ana kasoro mwilini mwake, ili kwamba asipanajisi mahali patakatifu pangu, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh anayewafanya watakatifu." \v 24 Kwa hiyo Musa akamwambia maneno haya Aroni, wanawe, na watu wote wa Israeli.