sw_lev_text_reg/21/10.txt

1 line
584 B
Plaintext

\v 10 Mtu ambaye ni kuhani mkuu miongoni mwa nduguze, ambaye mafuta ya upako yamekwisha kumiminwa kichwani pake, na ambaye amekwisha kuwekwa wakfu ili kuvaa mavazi maalum ya kuhani mkuu, kamwe hataziacha wazi nywele zake wala hatazirarua nguo zake. \v 11 Hataingia kamwe mahali popote ambapo kuna maiti na kujitia unajisi, hata kama ni maiti ya baba yake au ya mama yake. \v 12 Kuhani mkuu hataondoka eneo takatifu la hema la kukutania au kupatia unajisi patakatifu pa Mungu wake, kwa sababu amewekwa wakfu kuwa kuhani mkuu kwa kutiwa mafuta ya upako ya Mungu wake. Mimi ndimi Yahweh.