sw_lev_text_reg/08/28.txt

1 line
436 B
Plaintext

\v 28 Kisha Musa akaichukua mikate hiyo kutoka mikononi mwao na kuiteketeza juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Zilikuwa ni sadaka ya kuwekwa wakfu na ilitoa harufu ya kupendeza. Ilikuwa sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto. \v 29 Musa akakichukua kidari na kukitikisa kuwa sadaka ya kutikiswa kwa Yahweh. Ilikuwa ni mgao wa Musa wa kondoo wa kuwekewa mikono kwa makuhani, Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru yeye.