sw_lev_text_reg/13/56.txt

1 line
718 B
Plaintext

\v 56 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa, na kama ukungu umefifia baada ya kuwa umeoshwa, basi atakirarua kile kipande kilichochaufuliwa kutoka kwenye vazi au kutoka kwenye ngozi, au kutoka kwenye chombo kilichosukwa au kusokotwa. \v 57 Ikiwa ukungu unazidi kuonekana katika vazi, ama katika chombo kilichosukwa au kufumwa, au katika kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi, basi, ukungu utakuwa unasambaa. Kifaa chochote kilicho na ukungu ni lazima kichomwe. \v 58 Vazi au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi—iwapo unakisafisha kifaa nao ukungu ukawa umetoka, nacho kifaa lazima kisafishwe mara ya pili, kisha kitakuwa safi.