\c 4 \v 1 Bwana alisema na Musa na kumwambia, \v 2 "Waambie wana wa Israeli 'mtu yeyote akifanya dhambi bila kukusudia, kufanya chochote ambacho Bwana ameagiza kutofanya, na kama akifanya chochote kilichozuiliwa, yafuatayo lazima yatatendeka. \v 3 Kama ni kuhani mkuu aliyetenda dhambi na kuleta hatia kwa watu, atatoa dume asiyekuwa na kasoro kwa Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda kama sadaka ya dhambi.