sw_lam_text_ulb/02/11.txt

1 line
367 B
Plaintext

\v 11 Macho yangu yamekaukiwa machozi yake; tumbo langu la nguruma; sehemu zangu za ndani zimemwagika chini kwasababu ya uharibifu wa binti wa watu wangu, watoto na wachanga wamezimia mitaani mwa mji. \v 12 Wanasema kwa mama zao, "Mbegu ziko wapi na mvinyo?" kama wanavyo zimia kama mtu aliye jeruhiwa mitaani mwa mji, maisha yao yamemwagwa kwenye kifua cha mama zao.