\v 40 Natujichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Yahweh. \v 41 Na tunyanyue mioyo yetu na mikono yetu kwa Yahweh mbinguni: \v 42 "Tumekosea na kuasi, na haujasamehe. \v 43 Umejifunika na hasira na kutukimbiza, umeua na haujanusuru.