sw_jos_text_reg/10/01.txt

1 line
456 B
Plaintext

\v 1 Ikawa Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alisikia kuwa Yoshua ameiteka Ai na ameiteketeza kabisa, kama alivyokwisha kufaya huko Yeriko na mfalme wake. Na alisikia jinsi ambavyo watu wa Gibeoni walivyofanya amani na watu wa Israeli na walikuwa wanaishi miongoni mwao. \v 2 Watu wa Yerusalemu waliogopa sana kwasababu Gibeoni ulikuwa mji mkubwa, kama mmoja wa miji ya kifalme. Ilikuwa kubwa kuliko Ai, na watu wake wote walikuwa ni mashujaa wenye nguvu.