sw_jos_text_reg/21/43.txt

1 line
449 B
Plaintext

\v 43 Basi Yahweh aliwapa Israeli nchi yote ambayo aliwaapia baba zao kuwa atawapa. Waisraeli waliimiliki nchi na wakakaa humo. \v 44 Kisha Yahweh akawapa pumziko kwa kila upande, kama tu alivyowaahidia baba zao. Hakuna hata adui mmoja atakayeweza kuwashinda. Yawhew aliwatia maadui wao wote mikononi mwao. \v 45 Hakuna hata kitu kimoja miongoni kwa ahadi nzuri ambazo Yahweh alizisema kwa nyumba ya Israeli ambazo hazikutimia. Ahadi zote zilitimia.