sw_jos_text_reg/02/01.txt

1 line
467 B
Plaintext

\v 1 Kisha Yoshua mwana wa Nuni aliwatuma watu wawili kwa siri kama wapelelezi kutoka Shitimu. Akisema, "Nendeni mkaiangalie nchi, hasa Yeriko." Walienda na wakafika katika nyumba ya kahaba ambaye jina lake ni Rahabu, na wakalala hapo. \v 2 Mfalme wa Yeriko aliambiwa, "Tazama watu wa Israeli wamekuja kuipeleleza nchi." \v 3 Mfalme akatuma neno kwa Rahabu kusema, " Watoe watu waliokuja kwako ambao wameingia nyumbani mwako, kwa kuwa wamekuja kuipeleleza nchi yote."