sw_jos_text_reg/18/19.txt

1 line
407 B
Plaintext

\v 19 Mpaka ulipita hadi upande wa bega la kaskazini la Bethi Hogla. Mpaka ulikome katika ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, katika upande wa kusini mwishoni mwa Yordani. Huu ulikuwa ni mpaka wa upande wa kusini. \v 20 Yordani ulikuwa mpaka wake katika upande wa mashariki. Na huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Benyamini, na walipewa kwa kila ukoo wao, mpaka baada ya mpaka, kwa kuizunguka nchi yote.