sw_jos_text_reg/18/08.txt

1 line
510 B
Plaintext

\v 8 Hivyo, watu waliinuka na wakaenda. Yoshua akawaamuru wale walioenda kuandika maelezo ya nchi, akisema, "Pandeni juu na mshuke chini katika nchi na andikeni maelezo kuhusu nchi na kisha mrejee kwangu. Nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh huko Shilo. \v 9 Watu walienda na walitembea juu na chini katika nchi na wakaandika maelezo kuihusu nchi hiyo juu ya gombo kwa miji yake katika sehemu saba, kwa kutaja miji, kila mmoja katika sehemu moja. Kisha wakarudi kwa Yoshua katika kambi huko Shilo.