sw_jos_text_reg/14/13.txt

1 line
377 B
Plaintext

\v 13 Kisha Yoshua alimbariki Kalebu mwana wa Yefune na alimpa Hebroni kama urithi wake. \v 14 Hivyo Hebroni ikawa urithi wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi hata leo, kwasababu alimfuata kabisa Yahweh, Mungu wa Israeli. \v 15 Basi, jina la Hebroni hapo mwanzo lilikuwa ni Kiriathi Arba ( Arba ambaye alikuwa ni mtu mkuu miongoni mwa Wanakim). Kisha nchi ikawa na raha bila vita.