\v 4 Upigaji wa kura kwa ajili ya koo za Wakohathi ulileta matokeo haya: makuhani ambao ni wazawa wa Haruni ambao walitokana na Walawi, walipokea miji kumi na mitatu waliopewa kutoka kwa kabila la Yuda, kutoka kabila la Simoni, na kutoka kabila la Benyamini. \v 5 Koo zilizobaki za Wakohathi walipokea kwa kupiga kura kwa miji kumi kutoka katika kabila za Efraimu, Dani, na kutoka kwa nusu ya kabila la Manase.