\v 13 Kutoka hapo mpaka ulipita upande wa kusini katika mwelekeo wa Luzi (sehemu ile ile inayoitwa Betheli). Kisha mpaka ukashuka chini hata Atarothi Adda, karibu na mlima uliolekea kusini mwa Bethi Horoni. \v 14 Kisha mpaka ukaendelea upande mwingine: katika upande wa magharibi uligeukia upande wa kusini, ulienda mbele kuukabili mlima ulio ng'ambo ya Bethi Horoni. Mpaka huu ulikomea huko Kiriathi Baali ( ambao ndio Kiriathi Yearimu), mji ambao ulikuwa ni wa kabila la Yuda. Na huu ndio ulikuwa ni mpaka katika upande wa magharibi.