\v 6 Ndipo Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi alinena na kusema, "Mimi ni kijana mdogo, na ninyi ni wazee. Hii ndio sababu nilijizuia na sikuthubutu kuzungumza mawazo yangu mwenyewe. \v 7 Nilisema, "Urefu wa siku utazungumza; na wingi wa miaka utatufundisha hekima.