sw_jhn_text_reg/19/28.txt

1 line
376 B
Plaintext

\v 28 Baada ya hilo,huku Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, "Naona kiu." \v 29 Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake. \v 30 Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, "Imekwisha." Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.