sw_jhn_text_reg/05/01.txt

1 line
689 B
Plaintext

\c 5 \v 1 Baada ya hapo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, na Yesu alipanda kwenda Yerusalemu. \v 2 Na kule Yerusalemu palikuwa na birika kwenye mlango wa kondoo, lililokuwa likiitwa kwa lugha ya Kiaramu Bethzatha, nalo lina matao matano. \v 3 Idadi kubwa ya wagonjwa ilikuwemo, vipofu, viwete, au waliopooza walikuwa wamelala katika matao hayo. {Zingatia: Maneno ya mstari wa 3 hayaonekani katika nakala nzuri za kale. "Wakisubiri maji kutibuliwa.") Kwa hakikia wakati fulani malaika alishuka ndani ya Birika na kuyatibua maji. \v 4 Hivi kwamba, yule ambaye alikuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alifanywa mzima kutokana na chochote kilichokuwa kimemshika kwa wakati huo.