sw_jhn_text_reg/21/07.txt

1 line
479 B
Plaintext

\v 7 Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, "Ni Bwana." Naye Simon Petro aliposikia kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa vizuri), kisha akajitupa baharini. \v 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwenye mashua (kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni), nao walikuwa wakivuta zile nyavu zilizokuwa zimejaa samaki. \v 9 Walipofika ufukweni, waliona moto wa mkaa pale na juu yake kulikuwa na samaki pamoja na mkate.