sw_jhn_text_reg/21/01.txt

1 line
455 B
Plaintext

\v 1 Baada ya mambo hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi katika Bahari ya Tiberia; hivi ndivyo alivyojidhihirisha mwenyewe: \v 2 Simon Petro alikuwa pamoja na Thomaso aitwaye Didimas, Nathanaeli wa kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu. \v 3 Simon Petro akawaambia, "Mimi naenda kuvua samaki." Nao wakamwambia, "Sisi, pia tutaenda nawe." Wakaenda wakaingia kwenye mashua, lakini usiku huo wote hawakupata chochote.